Sunday, 4 May 2025

PDF File -WALIOITWA Kwenye Mafunzo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mei 2025

  AjiraLeo Tanzania       Sunday, 4 May 2025
WARNING
Beware of Job Scammers!
Please Never Pay Money To Get A Job!
PDF File -WALIOITWA Kwenye Mafunzo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mei 2025
Fire and Rescue Service
New Government Job Opportunities at Fire and Rescue Service May 2025

💥UNASUBIRI NINI? FOLLOW US ON INSTAGRAM. CLICK HERE!💥

AJIRA MPYA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI  TANZANIA 2025 | NAFASI MPYA ZA KAZI JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA 2025
PDF File -WALIOITWA Kwenye Mafunzo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mei 2025
Overview

Nafasi za Ajira Mpya JESHI la Zimamoto Tanzania Mei 2025, Ajira Mpya JESHI la Zimamoto Mei 2025, Ajira Mpya JESHI la Zimamoto Tanzania, Nafasi Mpya za Kazi JESHI la Zimamoto Tanzania Mei 2025, Tanzanian Fire and Rescue Force Jobs 2025, Ajira Mpya JESHI la Zima moto Tanzania Mei 2025, Ajira Mpya JESHI la Zima Moto Mei 2025, Ajira Mpya JESHI la Zima Moto Tanzania, Nafasi Mpya za Kazi JESHI la Zima Moto Tanzania Mei 2025

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

KUITWA KWENYE MAFUNZO YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatangaza majina ya waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Wahusika wote wanatakiwa kufika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga kuanzia tarehe 16 Mei, 2025 hadi tarehe 18 Mei, 2025 bila kukosa; kwa ambaye hatafika chuoni kwa tarehe zilizopangwa hatapokelewa na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.

Kufika chuoni shuka kituo cha Kabuku kilichopo kilometa 12 toka chuoni. Chuo kimeandaa utaratibu maalumu wa kuwapokea kwa tarehe zilizotajwa hapo juu, kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku.

Mhusika atapaswa kujigharamia nauli ya kwenda sambamba na chakula na malazi kwa siku zote ambazo atakuwa hajapokelewa Chuoni.
Mhusika anapaswa kuja akiwa na vyeti halisi vya masomo, taaluma au ujuzi alioombea pamoja na cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha NIDA au namba na leseni hai kwa walioomba nafasi ya udereva. Vyeti vyote tajwa hapo juu viwe na nakala tatu kwa kila cheti pia vyeti hivyo vitakaguliwa na kwa ambaye majina yake yatatofautiana kati ya vyeti vya shule/taaluma, NIDA na cheti cha kuzaliwa watarudishwa na nafasi zao zitachukuliwa na wengine.

Mhusika atakapofika chuoni awe tayari kupimwa afya ya mwili, akili na Mimba kwa wanawake na ambaye atabainika kuwa na kasoro za kiafyahataruhusiwa kuendelea na mafunzo na atarudishwa kwa gharama zake na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.

Wahusika wote wanatakiwa kuja na vifaa vifuatavyo: mashuka mawili (02) ya rangi ya bluu, mto 01 na foronya 02 ya rangi ya bluu, chandarua 01 rangi ya bluu (cha duara), ndoo ya plastiki ya lita 20, sahani na kikombe cha bati, fedha kiasi kwa matumizi binafsi na bima za afya kwa walionazo. Aidha vifaa vifuatavyo watanunua kwenye duka la Chuo, raba za michezo, fulana (T-shirt) rangi ya bluu, Madaftari makubwa (counter books 4 quire 5 pcs), vifaa vya michezo (truck suite, bukta bluu, na fulana) na kalamu.

PDF File -WALIOITWA Kwenye Mafunzo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mei 2025

DOWNLOAD PDF FILE YA MAJINA + MAELEZO HAPA!
logoblog

Thanks for reading PDF File -WALIOITWA Kwenye Mafunzo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mei 2025

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment