https://yas.co.tz/?utm_source=ssp&utm_medium=website&utm_campaign=yas+anzia+ulipo+campaign&utm_content=bluetrain

Wednesday, 6 August 2025

WAFCON 2024 - Taji la 10 kwa Nigeria, Morocco Washika Nafasi ya Pili kwa Mara ya Pili Mfululizo

  AjiraLeo Tanzania       Wednesday, 6 August 2025
WARNING
Beware of Job Scammers!
Please Never Pay Money To Get A Job!

WAFCON 2024 - Taji la 10 kwa Nigeria, Morocco Washika Nafasi ya Pili kwa Mara ya Pili Mfululizo

Taji la Kumi kwa Nigeria, Morocco Washika Nafasi ya Pili kwa Mara ya Pili Mfululizo: WAFCON 2024 Ilikuwa Sherehe ya Kandanda la Wanawake.

Mashindano ya timu bora za wanawake barani Afrika yalifanyika nchini Morocco. 1xBet, tovuti bora ya kubashiri michezo na mshirika rasmi wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), inatoa muhtasari wa mashindano haya.

Bora zaidi kati ya bora

Jumla ya timu 12 zilishiriki katika mashindano haya. Baada ya hatua ya makundi, timu 8 ziliingia robo fainali, ambapo mashindano halisi ya kuwania ubingwa yalianza. Morocco na Nigeria zilifika fainali bila kupoteza mchezo wowote, huku Ghana ikikutana na Afrika Kusini kwenye mechi ya kuwania nafasi ya tatu.

Pambano la nafasi ya tatu

Mechi ya kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu ilikuwa ya kuvutia na yenye msisimko. Afrika Kusini walimiliki mpira zaidi, lakini Ghana walionekana kuwa hatari zaidi kwa kuwa na nafasi nyingi za kufunga.

Goli la kwanza lilitokana na kosa la kipa wa Ghana, Cynthia Konlan, ambaye alishindwa kuhimili presha na kumpa mpinzani mpira. Nonhlanhla Mthandi alifunga kwa urahisi katika lango wazi na kuipa Afrika Kusini uongozi. Kipindi cha pili kikiwa kimefikia nusu, Ghana walifanikiwa kusawazisha kupitia kichwa cha Alice Kusi baada ya krosi kutoka wingi ya kushoto. Katika muda uliosalia, hakuna timu iliyoweza kupata ushindi, hivyo mshindi aliamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Ghana walikosa penalti yao ya kwanza, lakini walikusanya nguvu na kufunga zote zilizofuata. Wakati huo huo, wachezaji wa Afrika Kusini walikosa mara mbili. Hatimaye, Ghana walishinda mikwaju ya penalti 4–3, na kujipatia nafasi ya tatu barani Afrika, huku mabingwa watetezi wa awali wakishika nafasi ya nne.

Fainali yenye msisimko

Katika mechi ya mwisho, wenyeji Morocco walikabiliana na timu ya taifa ya Nigeria. Wakiwa na sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao, Morocco walishambulia tangu mwanzo na kufanikiwa kupata mabao mawili mapema. Ghizlane Chebbak alifunga bao la kwanza kwa shuti kali la mbali dakika ya 12, na muda mfupi baadaye, Sanaâ Mssoudy akaongeza bao la pili.

Nigeria walirejea mchezoni dakika ya 64 kupitia penalti iliyofungwa na Esther Okoronkwo. Dakika saba baadaye, Esther alimpa pasi nzuri Folashade Ijamilusi aliyefunga bao la kusawazisha. Dakika chache kabla ya mechi kumalizika, wasichana wa Nigeria walifunga bao la ushindi. Jennifer Echegini aliukwamisha mpira wavuni kwa Morocco baada ya kupokea pasi ndefu, na kuhitimisha ushindi wa kishujaa.

Ushindi huo wa mabao 3–2 uliiruhusu Nigeria kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya kumi katika historia. Morocco walikuwa karibu kupata taji lao la kwanza la bara, lakini walipoteza fainali kwa mara ya pili mfululizo.

Wachezaji Bora wa WAFCON 2024

Ghizlane Chebbak kutoka Morocco, aliyefunga mabao 5, alikua mfungaji bora wa mashindano haya. Jambo la kuvutia ni kuwa pia alikuwa mfungaji bora wa WAFCON 2022, alipofunga mabao 3, ingawa alishiriki nafasi hiyo na wachezaji wengine wawili. Kipa wa Nigeria, Chiamaka Nnadozie, alitajwa kuwa kipa bora wa mashindano, huku mchezaji mwenzake Rasheedat Ajibade, akitajwa kuwa mchezaji bora wa jumla wa mashindano.

1xBet, tovuti bora ya kubashiri michezo, ni mshirika rasmi wa CAF na inaunga mkono mashindano mbalimbali ya kandanda barani Afrika. Mashindano yajayo ya African Nations Championship (CHAN) pia yatafanyika kwa usaidizi wa chapa hii inayoaminika. Fuata matukio ya CHAN 2024 kuanzia Agosti 2 hadi 30, na fanya ubashiri wako kupitia tovuti ya 1xBet kwa kutumia kiungo:
👉 http://1xplayers.com/P9MMjHyT

logoblog

Thanks for reading WAFCON 2024 - Taji la 10 kwa Nigeria, Morocco Washika Nafasi ya Pili kwa Mara ya Pili Mfululizo

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment